MOYES ASAJILI BEKI WA KULIA TOKA ATLETICO MADRID
Kocha mpya wa Sunderland AFC David Moyes amekamikisha usajili wake wa 5 msimu huu akimsajili bekibwa pembeni kulia Javier Manquillo toka Klabu ya Atletico Madrid ya Hispania.
Mchezaji huyo mwenye miaka 22 anajiunga na Sunderland kwa mkataba wa mkopo wa msimu mzima kukiwa na kipengele cha kusajiliwa moja kwa moja.
Manquillo ambaye alishawahi kuichezea Liverpool msimu wa 2014/2015 katika mkataba wa mkopo wa msimu mzima anajiunga na Sunderland baada ya kumaliza msimu uliopita akicheza kwa mkopo katika klabu ya Marseille ya Ufaransa.
No comments