BAADA YA FRED, MAN UNITED YATANGAZA USAJILI WA BEKI


Siku moja baada ya kutangaza usajili wa Kiungo wa kimataifa wa Brazil, klabu ya Manchester United imetangaza usajili mwingine na sasa ni beki wa pembeni Diogo Dalot kutoka klabu ya FC Porto ya Ureno.

Kiasi cha paundi milioni 17.4 kimetumika kumsajili beki huyo wa kulia ambaye huchezea pia timu ya Taifa ya Ureno chini ya miaka 21 Kwa mkataba wa miaka mitano.

Nafasi ya beki wa kulia United ulikuwa ikijazwa na Antonio Valencia mwenye miaka 33 akisaidiana na Mateo Darmian lakini ujio wa Diogo Dalot unaweza kumkimbiza sasa Mateo Darmian anayetakiwa na Juventus.

No comments

Powered by Blogger.