Wapenda Soka Day


                                                                                                                        


Lengo kuu la Wapenda Soka (Kandanda) group ni kujadili mambo yote yanayohusiana na soka lakini sisi bado ni sehemu ya jamii na ni wajibu wetu kuisaidia jamii husika na ndipo tukaja na wazo la kutoa chochote kwa jamii hiyo na kila mmoja kwa uwezo wake na jinsi alivyoguswa na kutoa chochote.

SIKU YA WAPENDA SOKA NI NINI?
Hii ni siku maalumu ambayo wapenda Soka tulikubaliana ambapo kila MPENDA SOKA atakayejisikia atatoa chochote kwaajili ya kusaidia jamii hasa watoto yatima na kisha kukutana kwa pamoja siku hiyo kwenda kuwaona watoto Yatima.


SIKU YENYEWE NI LINI?
Siku ya Wapenda soka ni tarehe 1 January kila mwaka ambapo tunakutana na kujumuika na makundi haya maalum

UTARATIBU UKOJE?
kila MPENDA SOKA wa kundi hili anayejisikia ni wajibu wake kusaidia jamii tunaomba aguswe na kutoa chochote alicho nacho iwe nguo, Pesa, Chumvi, Mkate, mafuta n.k ikumbukwe wakati wewe una vingi kuna mtu hajui hata hiyo siku atakula nini .




No comments

Powered by Blogger.