ARSENAL YAMSAJILI MCHEZAJI MWINGINE KWA BEI KIDUCHU
Inaripotiwa kuwa Arsenal wamemsajili Kinda mwenye umri wa miaka 17, kiungo Yacine Adli kutoka PSG kwa ada ya £223,000
Mchezaji huyo anayecheza nafasi ya Kiungo alikataa ofa ya mkataba wa kusalia Paris Saint-Germain baada ya kupewa taarifa anatakiwa na boss wake wa zamani Unai Emery ambaye sasa anainoa Arsenal.
Taarifa zinasema Adli amesaini mkataba wa miaka mitatu ukiwa na chaguo la kuongeza mingine miwili iwapo kiwango chake kitaridhisha.
Inakumbukwa kuwa akiwa PSG, kocha Emery alimpa Adli nafasi ya kucheza kwa dakika saba katika mchezo wa Ligue 1 dhidi ya Caen.
Huu ni usajili wa pili wa kocha mpya wa Arsenal Unai Emery baada ya Jana kumsajili mlinzi Veterani raia wa Uswisi Stephan Lichtensteiner Kwa uhamisho huru na Leo wamemtangaza Adili Kwa pesa ndogo.
Inasemekana kocha wa Arsenal Unai Emery amekabidhiwa paundi milioni 50 pekee kuweza kuimarisha kikosi chake
No comments