BATSHUAYI ATIMKIA DORTMUND KUMPISHA GIROUD CHELSEA

Michy Batshuayi has undergone his medical at Borussia Dortmund ahead of loan switch 
Batshuayi akifanyiwa vipimo vya afya Dortmund
Mshambuliaji wa kimataifa wa Ubelgiji Michy Batshuayi amehama klabu hiyo na kujiunga na Borussia Dortmund ya Ujerumani kwa Mkopo wa miezi Sita.

Batshuayi anaondoka Chelsea kumpisha Olivier Giroud anayetarajiwa kusajiliwa leo siku ya mwisho ya usajili wa dirisha dogo nchini England na anaelekea Dortmund kuchukua nafasi ya Pierre-Emerick Aubameyang ambaye ametimkia Arsenal.

Chelsea tayari imelipa paundi milioni 18 kupata huduma ya mshambuliaji wa Arsenal Olivier Giroud baada ya kumkosa Edin Dzeko wa Roma ambaye usajili wake ulisitishwa siku chache zilizopita 

No comments

Powered by Blogger.