SIKU MOJA BAADA YA KUFUNGWA NA SWANSEA, ARSENAL YAMSAJILI AUBAMEYANG
Hatimaye klabu ya Arsenal imetangaza kumsajili mshambuliaji wa kimataifa wa Gabon aliyekua akiichezea Borussia Dortmund Pierre-Emerick Aubameyang kwa dau la uhamisho paundi milioni 56
Aubameyang mwenye miaka 28 hivi sasa anajiunga na Arsenal baada ya kukaa misimu mitano akiwa na Borusia Dortmund ambapo alifanikiwa kufunga magoli muhimu kwa klabu hiyo
Usajili wa mshambuliaji huyu unaongeza chachu katika safu ya ushambuliaji ya Arsenal na pengine akaleta kitu kipya baada ya Alexandre lacazette kutoonyesha yale makali yaliyotarajiwa.
Hii ni faraja kwa Mashabiki wa Arsenal ambao jana timu yao ilikumbana na kichapo cha bao 3-1 toka kwa Swansea katika mchezo wa ligi kuu ya England katika uwanja wa Liberty.
No comments