ARSENAL ILIVYOKARIBIA KUMNYAKUA FABINHO

Inaripotiwa kwamba Arsenal walijaribu kuingilia dili la uhamisho dakika za mwisho wakitaka kumnyakua Fabinho kabla hajatua Liverpool kutokea Monaco.
Inafahamika kuwa kiungo huyo mwenye umri wa miaka 24 anamvutia sana kocha mpya wa Arsenal Unai Emery ambaye alijaribu kumsajili wakati akiwa kocha wa PSG.
Sasa imefahamika kwamba Arsenal walifanya jaribio la kumnyakua mwishoni mwa juma lililopita lakini tayari Fabinho alikua amekwishaamua kujiunga na Liverpool.
Fabinho atajiunga rasmi na Liverpool mnamo Julai 1 baada ya kufuzu vipimo vya afya hapo jana.
Fabinho atajiunga na kikosi hicho katika siku ambayo pia Naby Keita atatua kutoka RB Leipzig.
Inafahamika pia kwamba Liverpool wapo mbioni kumsajili mshambuliaji wa Lyon Nabil Fekir japo mwenyewe amekaririwa akisema bado anahitaji muda kutafakari kuhusu 'future' yake.
No comments