RATIBA KAMILI YA SPORT PESA SUPER CUP

Michuano inayoshirikisha timu 8 inayodhaminiwa na kampuni ya mchezo wa kubahatisha Sportpesa ipo tayari kuanza kutimu vumbi huko Kenya, huku ikishirkisha timu kutoka Kenya na Tanzania.


Timu zitakazoshiriki Michuano hiyo ni pamoja na Kakamega Homeboys, Kariobang Sharks, Gor Mahia, AFC Leopard za nchini Kenya, na Tanzania ikiwakilishwa na  Simba, Yanga SC, Singida United na nafasi kutoka Zanzibar wakiwa ni vijana wa Jeshi La Kujenga Uchumi (JKU SC)

Ratiba kamili ya michuano hiyo ni kama ifuatavyo


Michuano kama hii ilifanyika mwaka jana 2017 na kushuhudia Gor Mahia wakitwaa ubingwa wa michuano hii. Baada ya ubingwa huo Gor Mahia wakapata nafasi ya kucheza na klabu ya Everton FC ya nchini Engand ilikuwa imesheeni mastaa kama Rooney n.k

Bingwa wa michuano hii mwaka huu atajizolea kitita cha pesa dolar za kimarekani 30,000, huku mshindi wa pili akiibuka na dola 10,000 na watatu akipata 7,500.

Watakaofanikiwa kuingia Nusu fainali watajipatia dola 5,000 kila mmoja huku kila timu ikipewa dola 2,500 kwa kuanzia hatua ya robo fainali.


No comments

Powered by Blogger.