HONGERENI SIMBA, ILA KIPIGO MLICHONIPA SITAKISAHAU - MASAU BWIRE

Baada ya timu yake kumaliza ligi kwa sare ya goli 1-1 dhidi ya Mbao FC, Msemaji wa klabu ya Ruvu Shooting Ameeandika waraka wa kuzisifu klabu zilizofanya vizuri katika ligi hii pendwa nchini Tanzania.
Ruvu Shooting wao wamemaliza ligi wakiwa na alama 38 zilizowawekwa nafasi ya 8 katika ligi kuu Vodacom Tanzania Bara.
Katika makala ndefu ambao amiandika Masau Bwire hakusita kuzimwagia sifa klabu za Simba SC, Azam FC na Yanga SC kwa kile walichochuma baada ya mechi 30 kumaliza za ligi kuu Vodacom Tanzania Bara.
Katika makala hayo, Bwire alianza kwa kuwapongeza Simba SC kwa kutoa Ubingwa wa na lakini akachagiza kutosahau kipigo cha 7-0 kutoka kwa Mabingwa hao wa ligi kuu bara. Masau Bwire aliandika "Ndugu wana soka, nawapongeza sana Simba SC kwa kumaliza ligi kwa mafanikio makubwa kwa kuchukua ubingwa ambao wameusotea kwa kipindi cha takribani miaka minne, hongereni sana Msimbazi japo mlitaka kuniua msimu huu maana kipigo mlichonipa si cha kukisimulia"
Lakini pia Masau Bwire aliendelea kuwatakiwa mema katika mashindano ya kimataifa Simba SC huku akiamini kuwa kama Simba SC wakijipanga Vizuri basi watafika mbali katika mashindano hayo ya kimataifa. Masau Bwire alisema katika makaya yake "Mnatuwakilisha kimataifa, ebu acheni mbwembwe, kuweni serious, mkatuwakilishe vyema."
Masau Bwire hakuishia hapo alienda mbele na kuwapongeza Azam FC kwa kukamata Nafasi ya pili katika ligi ukitofautisha na msimu mmoja nyuma. "Niwapongeze sana Azam ambao wamefanya vizuri sana msimu huu wa ligi 2017/18 kwa kuwa washindi wa pili ukilinganisha na msimu wa 2016/17 ambapo walishika nafasi ya nne, hongereni sana, mmepambana haswaaaa, ninyi ni wa kupigiwa mfano katika soka la nchi yetu, kwa kweli, hongereni sana" Alisema Bwire

Na kwanamna ya kipekee kabisa Masau Bwire alipongeza Klabu ya Yanga SC kwa kila jitihada na mapambano waliyoyafanya mpaka kufanikiwa kukamata nafasi ya tatu licha changamoto nyingi walizonazo. katika makala hiyo Masau Bwire Alisema "Pongezi za kipekee sana nawapatia washindi wa tatu, Young Africans (Msisitizo wa pongezi zangu). Hakuna asiyejua changamoto walizozipitia mabingwa hawa wa zamani, pamoja na hayo yote, walipambana kimya kimya, kiugumu ugumu, mpaka kumaliza ligi nafasi ya tatu".
Masau Bwire aliendelea kusisitiza kuwa kwa changamoto ambazo Yanga Walizozipitia na nafasi waliyoipata hakika wanastahili pongezi kweli kweli "hakika wanastahili pongezi kedekede, walifunga mikanda kweli kweli" ilisomeka sehemu ya makala hiyo ya Masau Bwire

Hakuishia hapo ila aliwaambia pia wale wanaibeza Yanga kwa kutokuchukua ubingwa msimu huu, wasisahau kuwa Yanga imechukua Ubingwa katika misimu mitatu mfulululizo kabla ya kuukabidhi kwa Watani wao wa jadi Simba SC. Katika makala hiyo Masau Bwire alidokeza kuwa hakuna timu inayoweza kuchukua ubingwa kila mwaka hivyo mafanikio waliyoyapata Yanga kwa misimu minne mfululizo hayatakiwi kubezwa kamwe.
Mwisho kabisa Masau Bwire hakuwaacha wana-Ruvu Shooting bila neno. Masau Bwire aliipongeza Ruvu Shooting, wachezaji pamoja na mashabiki na wale wote waliowaunga mkono kwa kufanikiwa kumaliza ligi wakiwa nafasi ya nane.
Masau Bwire Alimalizia kwa kusema "Kwa kauli mbiu ya 'kupapasa' timu hiyo ilitoa soka lenye kuonekana, safi na burudani kwa Watanzania na kusababisha kupendwa na kila kona ya nchi. Yaani, Ruvu Shooting raha sana, Tuliwapapasa kikamilifu".
No comments