HILI LITAMBAKIZA BALE REAL MADRID?
Gareth Bale anahusishwa na usajili wa gharama kubwa kuelekea Manchester United lakini staa huyo wa Wales ameshiriki katika uzinduzi jezi mpya za Real Madrid kwa msimu ujao.
Bale ameshiriki kikamilifu katika uzinduzi huo pamoja na Marcelo, Toni Kroos, Karim Benzema na Nacho Fernandez lakini kubwa linalozungumzwa ni kukosekana kwa Christiano Ronaldo katika uzinduzi huo.
Kukosekana kwa staa huyo wa Ureno kumeanza kuzua minong'ono hasa kuhusiana na alichokisema baada ya mchezo wa fainali ya ligi ya mabingwa mwishoni mwa juma lililopita
No comments