GIROUD AFIKIA REKODI YA ZIDANE TIMU YA TAIFA
Mshambuliaji wa kimataifa wa Ufaransa anayeichezea pia Chelsea ya England Olivier Giroud jana aliweza kufikia rekodi ya nahodha wa zamani wa Ufaransa Zenedine Zidane katika ufungaji wa mabao katika ushindi wa bao 2-0 walioupata Ufaransa dhidi ya Jamhuri ya Ireland
Mchezo huo wa kimataifa wa Kirafiki kujiandaa na fainali zijazo za kombe la dunia nchini Russia ambapo Giroud alifunga moja kati ya mabao hayo mawili ya Ufaransa huku Bao lingine likifungwa Nabil Fekir Kiungo anayewaniwa vilivyo na Liverpool.
Giroud amefikisha idadi ya mabao 31 katika timu ya Taifa Sawa na Zidane akiingia katika orodha ya wafungaji bora watano wa muda wote katika timu ya Taifa ya Ufaransa orodha inayoongozwa na Thierry Henry mwenye magoli 51.
WAFUNGAJI BORA UFARANSA
1. Thierry Henry: 51 goals (Michezo 123)
2. Michel Platini: 41 goals (Michezo 72)
3. David Trezeguet: 34 goals (Michezo 71)
4. Zinedine Zidane: 31 goals ( Michezo106)
5. Olivier Giroud: 31 goals (Michezo 72)
No comments