MAN CITY YAMSAJILI BONGE LA BEKI TOKA ATHLETIC BILBAO
Vinara wa Ligi kuu nchini England Manchester City wamevunja rekodi ya Usajili wao kwa kumsajili beki wa kimataifa wa Ufaransa Aymeric Laporte kutoka Athletic Bilbao Kwa ada ya uhamisho paundi milioni 57.
Laporte mwenye miaka 23 anakuwa mchezaji wa Kwanza wa Manchester City kusajiliwa kwa kiasi kikubwa cha fedha na amesaini mkataba wa miaka mitano na nusu akivunja rekodi iliyowekwa na Kevin De Bryune aliyesajiliwa kwa paundi milioni 55.
Laporte anayecheza nafasi ya beki wa kati anasajiliwa na kocha Pep Guadiola baada ya mawindo ya muda mrefu kutaka kumsajili mpaka ijumaa ambapo walifikia makubaliano ya kumsajili na leo Jumanne kutia saini mkataba wa kuichezea Manchester City.
No comments