AZAM, YANGA, DODOMA ZATINGA NANE BORA FA

Timu za Azam FC na Yanga zimetinga hatua ya nane bora ya michuano ya FA Cup baada ya kuibuka na ushindi katika michezo yake ya leo zikiwa ugenini.

Azam iliifunga Shupavu FC mabao 5-0 katika mchezo uliochezwa saa 8 mchana kwenye uwanja wa Jamhuri mkoani Morogoro.

Mshambuliji kinda Peter Paul alifunga hat trick akitokea benchi kuchukua nafasi ya Mbaraka Yusuph huku mabao mengine yakifungwa na Yahya Zayd na Idd Kipwagile.

Yanga nayo imetinga hatua hiyo kwa kuitoa Ihefu FC kwa mikwaju ya penati 4-3 baada ya kutoka sare ya bao moja katika muda wa kawaida.

Dodoma FC inayonolewa na kocha Jamhuri Kihwelo 'Julio' imeitinga nayo hatua hiyo baada ya kuifunga Mwadui FC mabao 2-1 katika uwanja wa Sokoine.

Kagera Sugar imetupwa nje ya michuano hiyo baada ya kukubali kipigo cha mabao 2-0 kutoka kwa Buseresele mtanange uliopigwa uwanja wa Kaitaba.

No comments

Powered by Blogger.