REAL MADRID YAMRUDIA DE GEA YAWEKA MEZANI PAUNDI MILIONI 60

Manchester United are braced for another attempt by Real Madrid to sign  David De Gea
Habari za ndani ya klabu ya Manchester United ambazo zimeripotiwa na vyombo vya habari leo ni kuhusu Real madrid kuanza tena mbio zao za kumsajili kipa namba moja wa United David De Gea.
Kiasi cha paundi milioni 60 kimewekwa mezani na mabingwa hao wa Ulaya ambao watakutana na Manchester United katika mechi mbili katika ziku chache zijazo moja ikiwa ni katika michuano ya International Champions Cup na nyingine ikiwa ni Uefa Super Cup ambayo itachezwa tarehe 8 mwezi ujao.

Manchester united wanataka kumbakiza de Gea mwenye miaka 26 hivi sasa huku mkataba wake ukiwa umebaki miaka miwili kuichezea United lakini ushawish wa fedha unaweza kuwafanya wakamwachia japo yaonekana si rahisi.

Manchester United na Real madrid zote ziko Nchini marekani hivi sasa zikijiandaa na msimu mpya wa ligi na michuano mbalimbali.

United ilimsajili David De Gea kwa paundi milioni 18.9 mwaka 2011 akitokea Atletico madrid 

No comments

Powered by Blogger.