CHALOBAH AIKACHA CHELSEA NA KUSAINI WATFORD MIAKA MITANO
Aliyekua kiungo wa Chelsea Nathaniel Chalobah ameikacha timu hiyo na kukubali kusaini kuichezea Watford inayoshiriki ligi kuu ya Engalnd kwa mkataba wa miaka mitano.
Kiasi cha paundi milioni 6 kimetajwa kama dau lililotumika kumhamisha mchezaji huyo aliyelelewa na Chelsea na kucheza mechi 10 tu za ligi akiwa na mabingwa hao wa ligi kuu ya England.
Chalobah ambaye huichezea pia England chini ya miaka 21 amegoma kusaini mkataba mpya na Chelsea na kuamua kutimkia mazima Watford lengo kuu ni kupata nafasi ya kucheza.
No comments