MAN CITY KUMFANYA WALKER KUWA BEKI GHALI ZAIDI DUNIANI
Manchester City wanakaribia kukamilisha usajili wa beki wa pembeni wa Tottenham Hotspur Kayle Walker kwa mkataba wa paundi milion 50 na likikamilika dili hili basi mchezaji huyu atakua ndiye beki ghali kabisa duniani kwa sasa baada ya John Stones ambaye alisajiliwa kwa paundi milion 47.5.
kiasi cha paundi milioni 45 zimetajwa kama usajili huku kukiwa na nyongeza ya paundi milioni 5 kama mchezaji huyo atafanya vyema.
Vipimo vya afya vinatarajiwa kuwa leo Ijumaa na pengine akatambulishwa baada ya majuma kadhaa ya tetesi.

No comments