RASMI: BAADA YA VIPIMO VYA AFYA SASA MORATA NI MCHEZAJI HALALI WA CHELSEA
Yametimia!
Baada ya kitendawili cha muda mrefu cha wapi staa wa Real Madrid Alvaro Morata ataelekea, hatimaye dau la £58 milioni limefanikiwa kumpeleka nyota huyo katika klabu ya Chelsea huku ikitarajiwa kuongezeka mpaka kufikia paundi milioni 70 kutokana na mafanikio atakayopata Chelsea.
Awali Morata mwenye umri wa miaka 24 aliripotiwa kutakiwa na Manchester United ambao walituma ofa kubwa zaidi ili kumnyakua lakini matajiri wa Real Madrid hawakua tayari kufanya biashara hiyo.
Baada ya kufuzu vipimo, sasa Morata anataraji kujiunga na kikosi cha Chelsea chini ya kocha Antonio Conte huko Singapore kuanzia wiki ijayo.
Itakumbukwa msimu uliopita Real Madrid walilazimika kumnunua nyota wao huyo kutoka Juventus ambako walimuuza awali na akiwa na Real Madrid alifanikiwa kufunga mabao 20 katika michezo 43 aliyocheza.

No comments