CAF YAONGEZA TIMU SHIRIKI AFCON,SASA MICHEZO KUCHEZWA JUNI


Inaweza kuwa fursa kwa nchi ambazo zimekua zikiyasikia kwenye bomba mashindano ya soka kwa mataifa ya Afrika (AFCON) kwa miaka mingi ikiwemo Tanzania ambayo ilishiriki kwa mara ya kwanza na ya mwisho mwaka 1980.

Sasa shirikisho la soka Afrika (CAF) limeamua kuongeza idadi ya timu hizo kutoka 16 hadi 24 kwa lengo la kuongeza mvuto na msisimko wa michuano hiyo.

Mabadiliko hayo yataanza mara moja katika michuano ya AFCON itakayofanyika mwaka 2019.

Mabadiliko mengine ni muhimu ni muda wa michuano hiyo ambayo imekua ikipigwa katika mwezi Februari, na sasa kuanzia mwaka 2019 itaanza kuchezwa katika kipindi cha mwezi June hadi Julai sawa na michuano mingine ya kimataifa.

1 comment:

Powered by Blogger.