NDIYO BASI TENA, CAF YAWANYANGANYA ZANZIBAR UANACHAMA.
Ile faraja na matumaini ya soka la Zanzibar kuanza kufaidi matunda ya kua mwanachama wa Shirikisho la soka barani Afrika, CAF, imezimika ghafla kama mshumaa leo baada ya CAF kutoa taarifa ya kuwanyang'anya uanachama huo.
Taarifa tuliyoipata kutoka CAF inasema waliipa Zanzibarb uanachama lakini kuna vigezo ambavyo Zanzibar haikidhi na havikuzingatiwa kwa sababu CAF haiwezi kuwa na wanachama wawili kutoka katika nchi moja.
Taarifa za ndani zaidi zinadai uanachama waliopewa CAF ulikua ni wa muda tu na ulihitaji ridhaa shirikisho la soka duniani FIFA ili uwe uanachama kamili, lakini FIFA hawajakubaliana na ombi hilo.
Uanachama wa Zanzibar umedumu kwa miezi minne tu tangu ulipotolewa na aliyekua Rais wa CAF Issa Hayatou.

No comments