MOURINHO AMGARAGAZA PEP GUADIOLA MAREKANI, LUKAKU NA RASHFORD WAINGIA KATIKA REKODI MPYA

Manchester United 2-0 Manchester City:
Pambano baina ya wapinzani wawili wa jiji la Manchester yani Manchester United na Manchester City limemalizika kwa United kuilaza man City bao 2-0 mchezo uliochezwa alfajiri ya leo kwa saa za hapa nyumbani ikiwa ni usiku jijini Huoston Marekani 


Mchezo huo wa kujiandaa na msimu pya wa ligi lakini pia kuwania ubingwa wa International Champions Cup ulikua ni wa kwanza kwa timu hizo kucheza nje ya England.

Mshambuliaji mpya wa timu hiyo Romelu Lukaku alitangulia kuipatia United bao la Kwanza kipindi cha kwanza dakika za mwisho huku Marcus Rashford akifunga bao la pili dakika moja baada ya kuingia bao la kwanza na kuwafanya wachezaji hao kuwa wachezaji wa kwanza katika historia ya mchezo huo kufunga magoli katika mechi ya kwanza nje ya England.

Man United imebakiza michezo miwili nchini Marekani dhidi ya Barcelona na Real Madrid katika michuano hiyo sawa na Manchester City. 

No comments

Powered by Blogger.