MORATA AWAAGA REAL MADRID MAZOEZINI TAYARI KUJIUNGA NA CHELSEA

Morata
Klabu ya Chelsea ya England ambao ndiyo mabingwa wa ligi kuu nchini humu wamekubaliana na Real Madrid kuhusu usajili wa Mshambuliaji Alvaro Morata ambaye amekamata vichwa vya habari vya magazeti na mitandano mbalimbali tangu dirisha la usajili lilipofunguliwa.


Kila Mpenda Soka aliamini kwamba Morata angejiunga na Manchester United na Romelu Lukaku angejiunga na Chelsea wakati zoezi la usajili lilipofunguliwa lakini imekua kinyume chake na jana Chelsea kupitia ukurasa wao wa twitter waliandika tayari wamefikia makubaliano ya kumsajili Mshambuliaji huyo zao la Real Madrid academy na msimu ujao tutamshuhudia akiichezea Chelsea

Akiwa mazoezini jana Morata alipata wasaa wa kuagana na makocha na wachezaji wenzake kabla ya kurudi Hotelini kujiandaa na safari ya kwenda London kwaajili ya vipimo vya afya na kusaini mkataba wa kuwatumikia mabingwa hao wa England.

Kiasi cha paundi milioni 70.6 kinatajwa kama ada ya uhamisho wa mchezaji huyo ambapo Chelsea watatoa paundi milioni 58 taslimu wakati huu na kisha kuongezea kadri atakavyokua akifanya vyema uwanjani.

No comments

Powered by Blogger.