HARAKA SANA, MTIBWA WAZIBA PENGO LA NDUDA.

Siku moja tu baada ya taarifa kutoka kwamba kipa wao namba moja, Said Mohamed maarufu kama Nduda amemwaga wino Simba klabu ya Mtibwa Sugar imeziba pengo lake.

Mtibwa wamemsajili tena golikipa wao wa siku nyingi, Shaban Hassan Kado kutoka Mwadui ya Shinyanga kwa mkataba wa miaka miwili.

Kado ambaye amewahi kuidakia timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars, amerejea Mtibwa ambako ndiko alikong'ara zaidi miaka saba iliyopita lakini amekua akitafuta maisha katika vilabu vingine kadha wa kadha.

Kado amewahi kuvichezea vilabu kama Yanga, Coastal Union na Mwadui, lakini Mtibwa pameonekana kama ndiyo nyumbani kwake kwani amekua akiingia na kutoka.

No comments

Powered by Blogger.