MONACO YAWASEMEA FIFA WANAOMSUMBUA MBAPPE.


Klabu ya Monaco imetuma malalamiko yake katika shirikisho la soka ulimwenguni, FIFA ikizilalamikia klabu za Manchester City ya England na PSG ya Ufaransa kwamba zimefanya mazungumzo na mshambuliaji wao Kyilian Mbappe bila idhini yao.


Mbappe mwenye umri wa miaka 18 amekua lulu kwa vilabu karibu vyote vikubwa barani Ulaya na vimekua vikipigana kumbo kumsajili.

Monaco wamesema vitendo vinavyofanywa na Man City na PSG ni kinyume na kanuni zinazosimamia soka nchini Ufaransa na duniani

Sheria za wachezaji wa kulipwa zinaikataza klabu kufanya mazungumzo ya usajili na mchezaji mwenye mkataba na timu nyingine bila idhini kutoka kwenye timu husika. Mbappe aliifungia Monaco mabao 27 msimu uliopita.

No comments

Powered by Blogger.