YANGA WASAJILI MCHEZAJI WA TANO, NI KINDA ASIYEFAHAMIKA.
Wakiwa mbioni kuachana na winga wao mwenye kasi, Saimon Msuva, Yanga wameamua kufanya jambo lisilotarajiwa na wengi.
Wameenda kwenye kambi ya timu iliyopanda daraja ya Lipuli FC ya Iringa, wakamtazama kijana Baruan Yahaya Akilimali ambaye amekua akijifua na kikosi hicho na kumsainisha mkataba wa miaka miwili.
Inadaiwa Yanga wamekua wakimfuatilia kinda huyo aliyehitimu masomo ya kidato cha sita mwaka jana huko nchini Uganda na taarifa zinasema alibaki kidogo kubadili uraia wake ili asalie nchini humo.
Baruan anakua mchezaji wa tano kusajiliwa na Yanga baada ya Ramadhan Shaibu, Youthe Roastand, Ibrahim Ajibu na golikipa kinda Ramadhan Kabwili.

No comments