SIMBA SASA WAMEAMUA, ERASTO NYONI NAE NDANI.


Unaweza kusema Simba wameamua na hawataki utani kabisa katika dirisha hili la usajili. Sasa hivi wapo katika kambi ya timu ya taifa, Taifa Stars na wanamsajili kila wanayemtaka.

Taarifa mpya sasa ni kwamba beki kiraka wa Taifa Stars kutoka Azam FC, Erasto Nyoni amejiunga na wekundu hao na amesaini mkataba wa miaka miwili.

Nyoni ni mchezaji mwandamizi katika kikosi cha Stars cha sasa akiwa amedumu tangu alipoitwa mwa mara ya kwanza na kocha mbrazil Marcio Maximo.

Wiki chache zilizopita, kiraka huyo alikua akitajwa kuwaniwa na Yanga ambao ni watani wa jadi wa Simba.

No comments

Powered by Blogger.