INTER MILAN YAMWEKEA NGUMU PERISIC KUJIUNGA NA MAN UNITED
Bosi wa Inter Milan, Luciano Spalleti amesema atakataa winga wake Ivan Perisic asiondoke klabuni hapo katika dirisha hili la usajili.
Perisic amekua akiwindwa na nashetani wekundu, Manchester United lakini Inter Milan wamekua wakiweka ngumu kumuuza nyota huyo raia wa Croatia.
Spalleti amesema kadri siku zinavyozidi kwenda, ndivyo inavyozidi kuwa vigumu kumpata mbadala wa Perisic hivyo iwapo itakuja ofa kwa ajili ya winga huyo, yeye ataikataa.
No comments