EL CLASICO YA KWANZA NJE YA SPAIN BAADA YA MIAKA 35, BARCELONA YAICHAPA REAL MADRID


Mchezo wa kirafiki wa kujiandaa na msimu mpya baina ya Real Madrid  na Barcelona umemalizika kwa Barcelona kuibuka na ushindi wa bao 3-2 mchezo uliochezwa usiku huu kwa saa za Africa Mashariki

Mchezo baina ya timu hizo hujulikana kama el Clasico na ni wa kwanza baada ya miaka 35 kuchezwa nje ya Spain ulishuhudiwa Nahodha wa Barcelona Lionel Messi alitangulia kuipatia Barcelona bao la kwanza dakika 3 tu baada ya kuanza kwa mchezo huo.

Dakika 4 baadae kiungo Ivan Rakitic aliipatia Barcelona bao la pili akiunganisha vyema mpira aliotengenezewa na Neymar lakini Mateo Kovacic alifanikiwa kuirudisha Real Madrid mchezoni akifunga bao dakika ya 14 kisha Marco Asensio kuisawazishia Real Madrid akifunga bao dakika chache kabla ya mapumziko.

Mpira wa adhabu ndogo uliopigwa na Neymar kipindi cha pili ulimkuta beki Gerard Pique aliyefunga kiulaini kuhakikisha ushindi kwa Barcelona

No comments

Powered by Blogger.