CHELSEA YAANGUKIA PUA KWA INTER MILAN YAPIGWA 2


Mabingwa wa ligi kuu ya soka nchini England klabu ya Chelsea imekumbana na kichapo cha bao 2-1 toka kwa Inter Milan kwenye mchezo wa mwisho wa michuano ya International Champions Cup huko Asia.

Juhudi kubwa zilizofanywa na winga wa Inter Milan ambaye anawindwa na Manchester United Ivan Perisic zilikua ni kero kwa mabeki wa Chelsea kwani walijikuta wakiruhusu mara nyingi mashambulizi hata upatikanaji wa bao la pili ambalo alillifunga kwa ustadi mkubwa baada ya goli la awali la Steven Jovetic 

Chelsea ilifanikiwa kupata bao la kufutia machozi lililofungwa na Kiungo wa Inter Milan  Geoffrey Kondobia bao ambalo liliwapa ahueni Chelsea japo halikuwanusuru kupata kichapo cha bao 2-1 ikiwa ni mechi yake ya mwisho barani Asia ambako waliweka kambi ya mazoezi 

No comments

Powered by Blogger.