LEICESTER CITY WAIPIGA CHINI OFA YA AS ROMA

Leicester City wameipiga chini ofa ya pili ya AS Roma ambao wanataka kumnunua kiungo wao mnyumbufu, raia wa Algeria  Riyad Mahrez.

Taarifa kutoka Italia zinasema ofa hiyo inakadiriwa kufikia £27 milioni baada ya ile ya mwanzo ya £20 milioni kukwaa kisiki siku chache zilizopita.

Mahrez ambaye alifunga mabao 10 katika michezo 48 msimu uliopita amekua akihusishwa na vilabu kadhaa baada ya kutamka mnamo mwezi Mei mwaka huu kwamba anataka kuihama Leicester.

No comments

Powered by Blogger.