GIROUD NA WENZAKE WAONGEZA MIKATABA KUBAKI ARSENAL


Arsenal imefanikiwa kuwaongeza mikataba wachezaji watatu wa kikosi cha kwanza wote wakitoka Ufaransa baada ya mazungumzo yaliyodumu kwa majuma kadhaa.

Wachezaji hao ni nahodha msaidizi Laurent Koscielny, Kiungo Francis Coquelin na mshambuliaji Olivier Giroud kwa miaka tofauti kwa kila mmoja huku mazungumzo ya kuwaongeza mikataba kiungo Mesut Ozil  na mshambuliaji Alexis Sanchez yakiendelea.

Laurent Koscielny mwenye miaka 31 amesaini mkataba mpya wa miaka mitatu na nusu mkataba utakaomalizika mwaka 2020 akitarajiwa kulipwa paundi 80,000 kwa wiki.

Olivier Giroud yeye amesaini mkataba mpya wa miaka miwili na nusu zaidi kubaki katika klabu hiyo akitarajiwa kulipwa paundi 90,000 mkataba utakaodumu mpaka mwaka 2019.

Coquelin yeye amesaini mkataba mpya wa miaka minne na nusu ambao unatarajia kumalizika mwaka 2021 na mshahara wa paundi 75,000.


No comments

Powered by Blogger.