ZLATAN IBRAHIMOVIC NDIYE MCHEZAJI BORA ZAIDI DISEMBA EPL
Mshambuliaji Zlatan Ibrahimovic ameshinda tuzo ya mchezaji bora wa mwezi Disemba katika ligi kuu ya England.
Zlatan ambaye amejiunga na Manchester United Msimu huu akitokea PSG baada ya kumaliza mkataba wake ameibuka na tuzo hiyo baada ya kungara vilivyo mwezi Disemba akiwa na Manchester United.
Amefanikiwa kufunga magoli matano mwezi huo wa Disemba na kuifanya United kushinda michezo yote iliyocheza mwezi huo na kutoka sare moja tu.
Zlatan alifunga katika sare ya bao 1-1 dhidi ya Everton, kisha akafunga bao la ushindi dhidi ya Crystal Palace wakati United iliposhinda bao 2-1 ugenini kisha akafunga mabao mawili wakati United ilipoibuka na ushindi wa 2-0 dhidi ya West Brom na kumalizia bao moja dhidi ya Sunderland wakati United ikishinda 3-1
Ibrahimovic anafunga mwaka 2016 kwa Tuzo hiyo baada ya Reheem Sterling kushinda August kisha Son Hueng-min kushinda Septemba,Eden Hazard kushinda Oktoba na Diego Costa kushinda Novemba


No comments