CONTE HII SASA SIFA: AWEKA REKODI MPYA TUZO YA MWEZI EPL
Kocha mkuu wa vinara wa ligi kuu ya England Klabu ya Chelsea Mtaliano Antonio Conte ametwaa tena tuzo ya kocha bora wa mwezi.
Conte ametwaa tuzo hiyo kwa mara ya tatu mfululizo msimu huu akifanya hivyo pia Oktoba na Novemba.
Conte anakuwa kocha wa kwanza katika historia ya ligi kuu ya England kushinda tuzo hiyo kwa mara tatu mfululizo.
Ushindi wa tuzo hiyo unatokana na mwendelezo mzuri wa ushindi akiiongoza Chelsea kushinda mechi 13 mfululizo.
Tuzo hizo 3 zinamfanya kumfikia Kocha Jose Mourinho ambaye ameshashinda tuzo hiyo mara tatu japo hakufanya hivyo mfululizo kama Conte na sio ndani ya miezi mitano kama ilivyo kwa Mtaliano huyo ambaye ameanza kibarua cha kuifundisha Chelsea msimu huu.

ORODHA YA MAKOCHA WALIOSHINDA TUZO HIYO MARA NYINGI
- 27 - Sir Alex Ferguson
- 15 - Arsene Wenger
- 10 - David Moyes
- 8 - Martin O'Neill,Harry Redknapp
- 6 - Sam Allardyce,Rafa Benitez na Bobby Robson
- 5 - Kevin Keegan,Claudio Ranieri
- 4 - Carlo Ancellot,Roy Hodgson,Joe Kinnear,Manuel Pellegrini na Gordon Strachan
- 3 - Allan Curbishley,Antonio Conte,Gerard Houllier,Ronald Koeman,Jose Mourinho,David O'Leary,Allan Pardew,Stuart Pearce,Mauricio Pochettino na Brendan Rodgers.

No comments