KUELEKEA KATIKA FAINALI ZA AFCON - HUU HAPA UCHAMBUZI WA MAKUNDI



Na Martin Kiyumbi.

GROUP A

GABON.

Hawa ndiyo wenyeji wa mashindano haya. Unaweza mwangalia Pierre- Emerick Aubameyang katika jicho la maendeleo zaidi.

Lakini kuna vitu ambavyo vinatia shaka kwa Gabon.

Cha kwanza wamemteua kocha wao mwezi mmoja kabla ya mashindano. Na kibaya zaidi ametoka kwenye mpira wa China na hajawahi kufundisha soka la Africa.

Hii inaweza ikampa ugumu kwa namna  mbili,  moja ugeni wa kikosi wa kikosi ambacho amekabidhiwa mwezi mmoja uliopita, pili ugeni wa soka la Africa pia inaweza ikawa kikwazo kwake.

Gabon kwenye mechi 13 zilizopita ameshinda mechi 2.Hii inaonesha wanapitia wakati mgumu sana katika kupata matokeo.

Mwaka  2013 hawakufuzu kwenda mashindano ya Afcon lakini mwaka 2015 walifuzu na wakaishia hatua ya makundi.

Mara ya mwisho kuandaa mashindano haya waliishia robo fainali. Mwaka huu pia Uwenyeji unaweza ukawabeba ukiachana na mchango mkubwa wa Pierre-Emerick Aubameyang. Wana nafasi kubwa ya kufuzu kwenye hatua  ya makundi.

CAMEROON

Sahau kizazi cha kina Eto'o , kuna kizazi kipya kinatengenezwa muda huu kwenye nchi ya Cameroon.

Wamefuzu kwenye michuano hii bila  kupoteza hata mchezo mmoja kutoka kwenye kundi lililokuwa gumu lenye timu za Afrika kusini,  Mauritania na Gambia.

Kitu kikubwa ambacho kitawateteresha na kuwafanya wasifike mbali kwenye mashindano haya ni kuwakosa nyota wake kama Matip ( Liverpool), Nyom ( Westbrom), Onana( Ajax), Assembe ( Nancy).

BURKINAFASO.

2010, 2012 na Mwaka  2015 walikomea Kwenye hatua ya makundi ya mashindano haya.

Mwaka 2013 waliishia nafasi ya pili. Kitu kikubwa ni kurejea kwa kocha wao Paulo Duarte ambaye walikuwa naye kuanzia mwaka 2008-2012.

Burkinafaso walikuwa hawakosi kushiriki michuano hii kwa sababu timu yao ilikuwa imejengwa na Paulo. Kurejea kwao kutakuwa msaada mkubwa sana kwao kwa sababu siyo mgeni wa timu hii.

GUINEA BISSAU.

Wamefuzu kwa mara ya kwanza, habari kubwa kwao siyo kufuzu kwa mara ya kwanza ila habari kubwa ni kundi ambalo walikuwepo mpaka wakafuzu michuano hii.

Congo ni wanarobo fainali wa mashindano yaliyopita,  wakati Zambia walikuwa mabingwa wa mwaka 2012 lakini waliweza fuzu mbele yao. Kwangu mimi Guinea Bissau ndiyo itakuwa Suprise package katika mashindano haya.


KUNDI B.


ALGERIA.

Hili ndilo kundi gumu kwangu na bingwa wa michuano hii atatoka kwenye group hili.

Algeria wanavipaji vingi sana kama kina Mahrez,  Slimani ( wote wametoka Leicester city) .Brahimi( Fc Porto), Bentaleb ( Schalke 04).
Hiki ndicho kizazi cha dhahabu kwao. Mashindano yaliyopita waliishia robo fainali.

TUNISIA.

Kwenye mashindano 7 wamefika robo fainali mara 5.

Uwepo wa Algeria kwenye group hili unatengeza mechi nzuri sana dhidi ya Tunisia na hii ni kwa sababu timu zote zimetoka Africa Kaskazini. Siku zote timu za Africa Kaskazini zinapokutana huwa kuna upinzani mkubwa.

Kwenye michezo 13 iliyopita Tunisia wameshindwa mechi moja tu,  hii inaonesha ni timu ambayo ni mshindi.

SENEGAL.

Kipi unakumbuka kuhusu Senegal?  Mimi kila ikitajwa Senegal  jina la nchi ya Uturuki huwa linakuja kwenye kichwa changu.

Wanarobo fainali wa kombe la dunia mwaka 2002 . Unakumbuka kizazi cha kina Alhaji Diouf?

Tayari kizazi hicho kimeshakufa, na muda huu kuna kizazi cha kina Mane ( Liverpool ), Kouyate( Westham), Diame.

Hawajawahi kushinda kombe hili. Wanakikosi kizuri sana Msimu huu. Kazi kubwa kwao ni kufuzu kundi hili, walifanikiwa kufuzu wana nafasi kubwa ya kwenda mbali.

ZIMBABWE

Wamefuzu kwa mara ya pili. Tayari bundi limeshaanza kuingia kwao.

Wachezaji walianza kugomea baada ya kucheleweshewa malipo yao na kudai pesa za motisha.

Hii kwa kiasi kikubwa kinaweza kuwatoa kwenye mchezo na ikizingatia wapo group gumu inaweza ikawa ngumu kwao kupita.

GROUP C.


IVORY COST.

Kuna vitu vingi sana vimebadilika sana kwenye kikosi cha Ivory Cost. Kizazi cha dhahabu cha kina Drogba,  Toure kimeshapita. Kocha wao Herve Renard ameshaondoka pia.

Herve Renard alikuwa mtu muhimu sana katika kuunganisha vipaji vya timu ya taifa ndiyo maana aliisaidia kuchukua ubingwa wa mwaka 2015.

Imefika fainali 3 katika mashindano 6 yaliyopita. Huwezi ipuuza hata kama kuna mabadiliko.

MOROCCO.

Herve Renard alishinda kombe hili akiwa na Zambia na Ivory Cost. Sifa kubwa ya Renard ni kuunganisha vipaji kwenye timu na kutengeneza timu imara ya ubingwa.

Ndiyo maana katika michezo 13 iliyopita Morocco hajafungwa hata mechi moja.
Tayari Renard ameshatengeneza timu imara. Naipa nafasi kubwa sana Morocco katika mashindano haya.

DR CONGO.

Mashindano yaliyopita walikuwa washindi watatu. Mashindano haya wanaingia bila ya nyota wao Bolasie. Mtihani mkubwa walionao ni kumfunga mmoja kati ya Morroco au Ivory Cost.
TOGO.
Mashindano yaliyopita hawakuwepo.

Hawana kikosi imara cha kutisha, wamekuwa hawana mwendelezo mzuri wa kiwango chao.

GROUP D.


GHANA.

Pamoja na wakati mgumu wanaopitia,  wamecheza mechi 5 bila ushindi.

Ila wanakikosi kizuri cha wachezaji kama kina Jordan na Andre Ayew.

Mashindano yaliyopita waliishia nafasi ya nne.Watamkosa Asmoah Gyan mwanzoni mwa mashindano haya.

MISRI.

Kufa kwa kikosi bora kilichochukua kombe mwaka 2006, 2008 na 2010. Taratibu Misri imeanza kuwekeza kwa vijana.

Mohamed Salah anarudi tena baada ya kukaa nje Kwa muda wa wiki tatu.

MALI.

Mashindano yaliyopita walikomea hatua ya makundi. Mashindano ya mwaka 2012 na 2013 waliishia nafasi 3.Kikosi chao hakijabadilika sana,  nawapa nafasi kubwa kwenye mashindano haya. Ni Suprise package yangu nyingine.

UGANDA.

Walishiriki  mara ya mwisho Mwaka  1978.Ni fahari ya Africa Mashariki kwa sasa.

Tuzo ya timu bora ya Africa inaweza ikaongeza morali kwenye kikosi chao.

Lakini kwangu mimi siwapi nafasi kubwa ya kufika mbali.

No comments

Powered by Blogger.