WENGER ASAJILI BEKI NA MSHAMBULIAJI, AMPELEKA CHAMBERS NA WILSHERE KWA MKOPO
Hatimaye Arsene Wenger amekata kiu ya mashabiki wa Arsenal kwa kufanya usajili wa wachezaji wawili wa nguvu.
Arsenal jana ilikamilisha usajili wa beki wa kimataifa wa Ujerumani Shkodran Mustafi kutoka Valencia ya Spain kwa paundi milioni 35.
Pia Arsenal jana ilitangaza pia kumsajili mshambuliaji Lucas Perez kutoka Deportivo La Coruna kwa ada ya uhamisho wa paundi milioni 17.
Mshambuliaji huyo raia wa Spain mwenye miaka 27 alifunga bao 19 akifunga bao 17 katika ligi kwa Deportivo msimu uliopita.
Wakati huo huo Beki Column Chambers na kiungo Jack Wilshere wameruhusiwa kuondoka klabuni hapo kwenda klabu nyingine kwa mkopo.
Chambers amejiunga na Middlesbrough kwa mkopo wa msimu mzima wakati Jack Wilshere anatarajia kujiunga na Crystal Palace kwa mkopo pia.

No comments