PSG WATAKA PESA ZAIDI KUMRUHUSU DAVID LUIZ KUTUA CHELSEA
Klabu ya Chelsea imekumbana na kikwazo toka kwa PSG katika usajili wa beki Mbrazil David Luiz baada ya mabingwa hao wa Ufaransa kutaka pesa zaidi.
Taarifa zinasema kwamba Chelsea walituma dau la paundi milioni 30 ambalo PSG wamelikataa na kuwataka Kuongeza ili wamruhusu beki huyo kuondoka Ufaransa.
Ikumbukwe kwamba PSG walimnunua David Luiz kwa paundi milioni 50 kutoka Chelsea na hawako tayari kupata hasara ya paundi milioni 20.
Tayari kocha mpya Chelsea Antonio Conte ameshaweka bayana nia yake ya kumsajili David Luiz baada ya kuwakosa mabeki wawili wa nafasi ya beki wa kati Romagnoli na Koulibaly.
David Luiz mwenye miaka 29 aliichezea Chelsea michezo 143 na kufunga mabao 22

No comments