BAADA YA JOE HART, MAN CITY YAWARUHUSU BONY,MANGALA NA NASRI PIA KUONDOKA
Siku moja baada ya Joe Hart kutimkia Torino ya Italia wachezaji watatu wameruhusiwa kuondoka leo kutoka katika klabu ya Manchester City.
Beki wa kati aliyenunuliwa kwa bei mbaya miaka miwili iliyopita Eliquim Mangala amejiunga na klabu ya Valencia ya Spain kwa mkopo wa msimu mzima.
Kiungo Samir Nasri nae amefanikiwa kukamilisha usajili wake kwenda Sevilla ya huko huko Spain kwa mkopo wa msimu mzima katika klabu ambayo inashiriki katika ligi ya mabingwa barani Ulaya.
Mshambuliaji Wilfried Bony ambaye hakupata mafanikio akiwa na Manchester City kama ilivyokua katika klabu ya Swansea nae ameruhusiwa kujiunga na Stoke City kwa mkopo wa msimu mzima.
Mchezaji ambaye amebaki klabuni hapo huku mustakabali wake ukiwa haujajulikana ni Yaya Toure ambaye hakuna taarifa yoyote inayomhusisha na kuihama klabu hiyo kabla ya kufungwa kwa dirisha la usajili usiku wa leo.

No comments