MOYES ASAJILI WAWILI TOKA MAN UNITED, AMTAKA PIA JANUZAJ KWA MKOPO

Kocha mkuu wa Sunderland David Moyes ameendelea kukijenga kikosi chake kwa kusajili wachezaji wawili toka katika klabu yake ya zamani Manchester United.
Mabeki wawili vijana Donald Love na Paddy McNair wamesaini kuichezea Sunderland toka katika academy ya Manchester United wote wana miaka 21.

Sunderland imelipa kiasi cha paundi milioni 5.5 kuwapata wachezaji wote hao wawili wakisaini kuichezea klabu hiyo kwa mkataba wa miaka minne kila mmoja.

Wakati huo huo Adnan Januzaj atajiunga na Sunderland muda wowote kuanzia sasa kwa mkopo baada ya kukataliwa kujiunga moja kwa moja na hii inatokana na Kocha Jose Mourinho kuamini kwamba kuna kitu kizuri kwa kijana huyu toka Ubelgiji.

No comments

Powered by Blogger.