MUSA MGOSI ASTAAFU KUAGWA JUMAPILI, MKUDE NAHODHA MPYA SIMBA,MWALYANZI APELEKWA AFRICAN LYON

Aliyekua nahodha wa Simba Mussa Hassan Mgosi ameamua kustaafu rasmi kucheza soka na sasa amepewa kazi mpya ndani ya Simba.


Taarifa ya Afisa Habari wa klabu hiyo Haji Manara inasema kwamba Mgosi sasa atakua ni Meneja wa timu ya Simba na sio mchezaji tena wa Simba.

Nafasi ya Unahodha wa Simba sasa itachukuliwa na Jonas Mkude aliyekua nahodha msaidizi huku Mgosi akitarajiwa kuagwa Jumapili katika mechi dhidi ya URA Ya Uganda pambano litakalopigwa katika dimba la Taifa jijini.

Katika hatua nyingine kiungo wa timu hiyo Peter Mwalyanzi ambaye alisajiliwa msimu uliopita toka Mbeya City amepelekwa kwa Mkopo katika Klabu ya African Lyon ya Dar es Salaam.

"Simba imekua na wachezaji wengi katika nafasi ya kiungo hivyo Mwalyanzi anapelekwa kwenda kulinda kiwango chake na kama kocha ataridhia arudishwe atarudishwa" ilisema taarifa hiyo ya Manara.

No comments

Powered by Blogger.