DONALD NGOMA KUIKOSA MO BEJAIA JUMAMOSI

Mshambuliaji wa kimataifa wa Zimbabwe na klabu ya Yanga Donald Ngoma ataikosa mechi ya Jumamosi dhidi ya MO Bejaia ya Algeria.


Pambano hilo litakalopigwa katika dimba la Taifa jijini Dar Es Salaam ni la marudiano baina ya timu hizo katika michuano ya kombe la shirikisho barani Afrika

Donlad Ngoma mshambuliaji tegemezi wa Yanga ataikosa mechi hiyo kwakua na kadi mbili za njano akiungana pia na Geoffrey Mwashiuya ambaye ni majeruhi pekee katika kikosi cha Yanga.

Tayari MO Bejaia wako Dar es Salaam wakifikia katika hoteli ya Ledger Plaza nje kidogo ya jiji la Dar.

No comments

Powered by Blogger.