MAN CITY YAKAMILISHA USAJILI WA LEROY SANE TOKA SCHALKE 04

Klabu ya Manchester City imekamilisha usajili wa winga Leroy Sane kutoka klabu ya Schalke 04 ya Ujerumani.


Dau la paundi milioni 37 limelipwa na Manchester City dau ambalo linaweza kupanda mpaka paundi milioni 42.

Sane mwenye miaka 20 amesaini mkataba wa miaka mitano kuichezea Manchester City na amekabidhiwa jezi namba 19.

Mchezaji huyo ambaye huichezea pia timu ya taifa ya Ujerumani anakua mchezaji wa 6 kusajiliwa na kocha mpya wa klabu hiyo Pep Guadiola.

No comments

Powered by Blogger.