YANGA NIA WANAYO,UWEZO WANAO LAKINI MIPANGO NDIO MMMH.

Na Chicharito G.

Kocha wa kihistoria wa Liverpool William "Billy" Shankly aliwahi kusema "Nashangaa wale wanaosema mchezo wa mpira ni mchezo wa maisha na kifo. Mimi ni mtu tofauti na wao sababu mchezo wa mpira ni zaidi ya hivyo vyote".


Baadae aliibuka kocha wa zamani wa Nottingham Forest Brian Clough alisema "Naamini kupitia maajabu". Hao wote ni makocha wawili walioamini kupitia kile walichosema na walitumia maneno yao kujenga timu zao.

Unadhani Hans van Pluijm wa Yanga atakuwa hana kauli yake ambayo amewalisha wachezaji wake!!? Siamini sana katika hilo sababu timu zetu hawapendi kuweka mambo yao wazi.

Tangu kocha wa Yanga aingie kwenye timu ameifanya Yanga iwe timu bora maradufu zaidi ya miaka 3 nyuma. Pamoja na kuitengeneza Yanga bado kuna kitu wanakikosa ambacho kitawafanya waongee lugha moja.

Yanga nia wanayo wamejitahidi kufika hapa walipo sababu walikuwa na nia ya kufanikisha mipango yao. Uwezo wanao sababu kwa upande wa uwanjani wamekuwa tofauti sana mpira unachezwa zaidi lakini Malaika wa bahati amekuwa mbali nao. Tatizo kubwa la Yanga ni mipango hafifu.

Waarabu wameshafahamu hakuna timu nyonge tena sasa. Wanachofanya ni kutumia mipango thabiti ya kutumia udhaifu wa timu wanazokabiliana nazo na hiyo yote ni baada ya kufanya uchunguzi wakina.

Yanga katika mechi zao zote za Kimataifa wamekuwa na makosa yale yale ambayo kiufundi yanaweza kutafutiwa majibu. Ni wazi upande wa Kushoto umekuwa dhaifu na njia ya wapinzani katika kuishambulia Yanga. Kwa mchezo uliopita tuliona Nadir Haroub akipangwa na Yondani lakini jibu lililotokea swali lake lilikuwa inakuwaje Nadir anacheza mechi muhimu huku akiwa hana match fitness!!? Ni kamari ambayo Hans aliicheza vibaya. Vincent Andrew wengi mnamwita Dante huu ni muda wake wa kuaminiwa hili aingie kwenye mfumo wa timu.

Pamoja na Yanga kucheza soka la kumiliki wamekosa muunganiko sahihi wa viungo wa kati. Kamusoko haendani na Twite muunganiko wao unaleta mashaka sababu wameshindwa kujipanga na kujiongoza wenyewe. Sio lazima waongee sababu mpira una lugha yake na njia zake. Ni vyema zaidi Yanga wakitumia kiungo asilia wa kuzuia hapa na maanisha kiungo mkabaji.

Katika idara ya ushambuliaji kuna machaguo mengi ambayo yanajitosheleza. Wengi wamekosa imani na Chirwa ambaye ni ingizo jipya,tukumbuke Chirwa anahitaji muda zaidi wa kuingia kwenye mfumo wa Yanga pia ameingia Yanga wakati wakiwa kwenye mashindano yenye presha zaidi.

Kwangu mimi hakuna walichokipoteza Yanga zaidi wanatakiwa kujivunia hatua ambayo wameifikia mpaka sasa tofauti na huko walikotoka kwenye mashindano ya kimataifa kwani mpaka sasa timu gani itapangiwa yanga isiogope kwa timu za afrika?

Ni vizuri zaidi kama Yanga wataamua kwenda sambamba na mwalimu pamoja na benvhi zima la ufundi kukaa na kutatua mapungufu yote yaliopo kwenye timu mapema kabla dirisha la usajili halijafungwa.

Yanga pia wanapaswa kufahamu kuwa mpira wa sasa ni wa ushindani na wamatokeo haswa pale unapokuwa na mechi nyumbani kwako kwani kwakweli hili limekuwa tatizo kwa vilabu vyote vya nchi yetu hata timu ya taifa swala la matumizi bora ya ardhi ya nyumbani imekuwa tatizo.

Pia kuna hili swala la wachezaji wanaosajiliwa kwenye kujaza mapengo au mapungufu ya timu nawaomba wana yanga pamoja na viongozi tulete watu sahihi na watu bora sio bora watu.

Naaamini kwa kuyazingatia haya basi yanga naiona mbali sana mwakani kwenye mashindano yajayo ya kimataifa.

Naipenda sana Yanga Yangu.

Mungu ibariki Yanga

Mungu ibariki Tanzania.

No comments

Powered by Blogger.