MO ATOA MILIONI 100 KUSAIDIA USAJILI SIMBA

Siku chache baada ya kuridhia mabadiliko ya mfumo wa uendeshaji wa klabu ya Simba Mohamed Dewji maarufu kama MO ametoa cheki ya milioni 100 kusaidia usajili katika klabu ya Simba.


MO alimkabidhi hundi hiyo Rais wa Simba Evans Aveva ikiwa ni ahadi yake ya kusaidia usajili ndani ya Simba.

Aveva alimshukuru MO na kusema kwamba pesa hizo zitasaidia katika bajeti ya milioni 420 ya klabu hiyo katika usajili msimu huu.


No comments

Powered by Blogger.