BAADA YA SIMBA KURIDHIA MABADILIKO, YANGA NAO KUKUTANA JUMAMOSI

Siku mbili baada ya wekundu wa Msimbazi Simba kuridhia mabadiliko ya mfumo wa uendeahaji wa klabu hiy Uongozi wa mabingwa wa soka Tanzania bara Yanga nao umeitisha mkutano mkuu wa wanachama.



Katika nakala ya Tangazo la mkutano huo ambayo WapendaSoka imefanikiwa kuipata Uongozi wa Yanga umeitisha mkuano mkuu wa wanachama wote utakaofanyika jijini Dar Es Salaam

Barua hiyo iliyosainiwa na katibu mkuu wa klabu hiyo Baraka Deusdedit inataja kuwa mkutano huo utafanyika katika ukumbi wa Diamond Jubulee jijini Dar es Salaam siku ya Jumamosi Tarehe 6 Agosti 2016 kuanzia saa 3 kamili asubuhi.

Barua hiyo haijataja Agenda ya mkutano huo lakini wadadisi wa maswala ya soka wanataja Mabadiliko kama moja ya hoja siku hiyo.

Pia siku hiyo utapigwa mchezo wa kirafiki kati ya Yanga na Mtibwa Sugar katika dimba la Taifa Jijini Dar kuanzia saa 10 jioni.


No comments

Powered by Blogger.