BLASZCZYKOWSKI ASAINI MIAKA MITATU WOLFSBURG

Kiungo wa kimataifa wa Poland aliyekua akiichezea Borussia Dortmund Jakub Blaszczykowski amesaini kuichezea Wolfsburg.


Kiungo huyo mwenye miaka 30 amesaini mkataba wa miaka mitatu kuichezea Wolfsburg inayoshiriki pia ligi kuu ya Ujerumani Bundesliga mkataba utakaomweka katika klabu yake hiyo mpya mpaka mwaka 2019.

Kiasi cha paundi milioni 4.2 ndizo zilizomng'oa Jakub kutoka Borussia Dortmund ambako alipata mafanikio ya kushinda ubingwa wa Bundesliga mara mbili mwaka 2011 na 2012.

Msimu uliopita alicheza kwa mkopo Fiorentina ya Italia na ni mmoja wa wachezaji waliofanya vizuri akiwa na kikosi cha Poland.


No comments

Powered by Blogger.