SIMBA YAENDELEZA VIPIGO MOROGORO, BUKINAFASO WAPIGWA "MKONO"

Wekundu wa Msimbazi Simba wameendeleza dozi katika mechi zake za kujiandaa na msimu mpya baada ya kuifunga Bukinafaso bao 5-0.


Mchezo huo uliopigwa mjini Morogoro ulikua ni wa tatu kwa Wekundu hao wa Msimbazi ambao jana kwa sauti moja waliridhia mabadiliko ya mfumo wa uendeshaji wa klabu hiyo.

Ibrahim Ajib alipiga mabao mawili tena leo kama ilivyokua katika mchezo dhidi ya Polisi Morogoro huku Moussa Ndusha kutoka Congo DR,Shiza Kichuya na Said Ndemla wakifunga bao 1 kila mmoja.

Simba ilianza mechi za maandalizi kwa kushinda bao 6-0 dhidi ya Polisi Morogoro kabla haijaifumua Moro Kids bao 2-0 na leo Bukina faso bao hizo 5-0.

KIKOSI CHA SIMBA KILICHOANZA LEO

1.Vicent Angban
2.Malika Ndeule
3. Mohammed Hussein "Zimbwe Jr".
4.Mwanjali
5.Juuko Murshid
6. Jonas Mkude
7.Mwinyi Kazimoto
8.Mohamed Ibrahim
9. Ibrahim Ajib
10. Moussa Ndusha
11. Peter Mwalyanzi

No comments

Powered by Blogger.