BAADA YA KUSHINDIKANA UJERUMANI BENDTNER KUPEWA NAFASI QPR

Kocha mkuu wa Queens Park Rangers Jimmy Floyd Hasselbaink amemgeukia mshambuliaji wa zamani wa Arsenal na timu ya taifa ya Denmark Nicklas Bendtner.


Mchezaji huyo yuko huru sasa baada ya kutupiwa virago na klabu ya Wolfsburg ya Ujerumani aliyokua akiichezea mpaka mwanzo wa mwaka huu.

Bendtner ana miaka 28 tu lakini imekua ngumu kwake kupata timu ya kuichezea kutokana na utovu wa nidhamu na Hasselbaink anaonekana kama anataka kujaribu kumrekebisha na kuisaidia QPR katika kampeni zake za kusaka nafasi ya kupanda daraja.

 Bendtner ameichezea Wolfsburg michezo 13 katika ligi kuu ya Ujerumani akifunga mabao mawili tu.

No comments

Powered by Blogger.