ASAMOAH GYAN AREJEA ENGLAND NA KUJIUNGA NA JAAP STAM
Nahodha wa Ghana Asamoah Gyan amejiunga na klabu ya Championship ya Reading FC ya nchini England kwa mkopo wa msimu mzima.
Reading ambayo inafundishwa na mlinzi wa zamani wa Manchester United Jaap Stam imemsajili kwa mkopo mchezaji huyo toka katika klabu ya ligi kuu ya China Shanghai SIPG.
Gyan mmoja kati ya wachezaji wanaolipwa pesa nyingi sana duniani amekubali kutimkia England baada ya kuambiwa hana nafasi huko China na inasemekana Reading watamlipa paundi 50,000 kwa wiki katika mshahara wake wa paundi 227,000 kwa wiki huku malipo yaliyobaki yakilipwa na Shaghai SIPG.
Hii ni mara ya pili kwa nyota huyo mwenye uwezo mkubwa wa kufunkucheza England baada ya kuichezea Sunderland kabla na hatimaye kutimkia Uarabuni.

No comments