BAADA YA KUWABANIA SIMBA, KIPA JKT RUVU AITWA TAIFA STARS

Kocha Mkuu wa timu ya Mpira wa Miguu Tanzania ‘Taifa Stars’, Charles Boniface Mkwasa, amefanya mabadiliko kwenye kikosi kinachotarajiwa kusafiri Jumatano Agosti 31, 2016 kwenda Nigeria kwa ajili ya mchezo wa mwisho wa kuwania kucheza fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON 2017) dhidi ya timu ya taifa ya nchi hiyo, Super Eagles.



Mabadiliko yaliyofanyika ni kwa kumchukua Kipa kinda wa JKT Ruvu, Said Kipao kuchukua nafasi ya Deogratius Munishi ambaye amefiwa na baba yake mzazi katika kifo kilichotokea jijini Dar es Salaam jana Agosti 28, 2016.
Licha ya mchezo huo wa Septemba 3, 2016 kuwa sehemu ya mchuano wa kuwania nafasi ya kucheza fainali hizo za AFCON 2017 huko Gabon, lakini utakuwa ni wa kukamilisha ratiba baada ya Misri kufuzu kutoka kundi G ambalo mbali ya Nigeria na Tanzania, pia ilikuwako Chad ambayo iliyojitoa katikati ya mashindano.
Wachezaji wanaounda kikosi hicho kwa sasa na kuanza kuingia kambini Hoteli ya Urban Rose jijini Dar es Salaam ni:

Walinda Mlango:
Said kipao, Aishi Manula.

Walinzi:

 Kelvin Yondani, David Mwantika, Vincent Andrew,  Shomari Kapombe, Mwinyi Haji, Mohamed Hussein.

Viungo:
 Jonas Mkude, Himid Mao, Muzamiru Yassin, Shiza Ramadhan, Farid Mussa, Simon Msuva.Ibrahim Jeba

Washambuliaji:

 John Bocco, Mbwana Samatta, Ibrahim Hajib.Jamal Mnyate

No comments

Powered by Blogger.