PAUNDI MILIONI 100 KWA POGBA? UTANI HUU! ~ ASEMA SCHOLES

Sakata la usajili wa kiungo wa kimataifa wa Ufaransa na klabu ya Juventus limezidi kushika kasi baada ya wadau mbalimbali duniani kupondea kiasi cha Fedha ambacho kinatajwa kama thamani ya mchezaji huyo.



Moja ya watu hao ni Kiungo wa zamani wa Manchester United Paul Scholes ambaye amefunguka na kusema itakua utani kwa Klabu yake hiyo ya dhamani kumnunua Paul Pogba kwa Paundi milioni 100.

Scholes anasema thamani ya Pogba inaweza kufikia paundi milioni 86 tu kama akijitahidi kufanya vizuri zaidi lakini si zaidi ya hapo.

Scholes anaamini mchezaji mwenye thamani hiyo ni kama Ronaldo au Messi ambao kila msimu una uhakika wa kupata goli zaidi ya 50.

Scholes alicheza na Pogba wakati wakiwa United na anaamini aliachwa kwakua alitaka pesa nyingi zaidi wakati hakua katika kikosi cha kwanza.

Bado Haijajulikana mustakabali wa Mchezaji huyo kama atasajiliwa na United au hapana.

1 comment:

Powered by Blogger.