AMERUDI : DAVID MOYES KOCHA MPYA WA SUNDERLAND

Aliyekua kocha wa Everton na Manchester United David Moyes ameteuliwa kuwa kocha mkuu wa Sunderland.


Moyes amesaini mkataba wa kuifundisha Sunderland kwa miaka minne akichukua nafasi ya Sam Allardyce aliyeteuliwa kuwa kocha mpya wa timu ya Taifa ya England.

Tangu alipotimuliwa kuifundisha Real Sociedad ya Spain Moyes mwenye miaka 53 hakupata timu ya kuifundisha licha ya kuhusishwa na klabu mbalimbali.

Moyes ambaye ameshafundisha michezo 845 tangu aanze kufundisha soka akishinda michezo 370,amedroo michezo 221 na kupoteza michezo 254 akiwa na asilimia za ushindi 43.79%

No comments

Powered by Blogger.